Kisonono ni
nini?
Kisono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya
Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukua na kuzaliana kwa haraka katika
sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa
wanawake (cervix)
Mirija ya kupitisha mkojo au mbegu za kiume
(urethra), mdomoni na kwenye puru au rectum. Maambukizi mengi kwa wanawake
hutokea kwenye shingo ya kizazi. Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono huwapata watu
wenye umri wa kati ya miaka kati 15 hasi 29
Ambapo
wanawake walio katika umri wa miaka 15
hadi 19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 hadi 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata
ugonjwa huu. Hii inaonesha kuwa ugonjwa wa kisonono huwapata zaidi vijana.
Je, Ugonjwa
wa gono huambukizwa vipi? Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kutoka kwa mtu
utakayejamiiana naye kupitia uke, njia ya haja kubwa na kupitia mdomo. Ugonjwa
huu unaweza kujitokeza kwenye sehemu za siri, kwenye mdomo na kwenye puru au
recktamu.
Pia
mama mjamzito mwenye kisonono anaweza kumuambukiza mwanaye wakati wa
kujifungua. Licha ya ugonjwa wa gono kuonekana sana miongoni mwa vijana, pia
unaonekana kwa watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu
wenye asili ya Afrika na watumiaji madawa ya kulevya.
0 comments: