Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia
ushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza
kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha
na kushindwa hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele.
Wanye tabia ya kushindwa kimaisha
hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda
mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na
kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha.
Ukitaka
kuwa mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi maisha
ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.
0 comments: