Utafiti unaonyesha wanaume wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya kuepuka kensa ya tezi la kibofu cha mkojo Kahawa ni kinywaji kikubwa katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya...
Utafiti mpya uliofanywa kwa kushirikisha wanaume
elfu 50 unasema kuwa watu wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya
kuepukana na saratani au kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
Kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kumekuwa na imani kuwa
unywaji kahawa unasaidia katika kuepusha kensa hiyo, lakini katika tafiti huu
mpya wanasayansi wanasema wamegundua tofauti kubwa katika kuepusha saratani
kali.
Mwanasayansi Kathryn Wilson wa Idara ya afya ya umma
ya chuo kikuu cha Havard nchini Marekani anasema "wanaume wanaokunywa
vikombe sita au zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa
hiyo kwa asilimia 60 ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa."
Kahawa ina kemikali mbali mbali, ikiwa na
viambatisho vinavyopambana na magonjwa na hiyo huenda ni pamoja na kemikali
zinazozuia kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
Kensa hiyo ni ya pili kwa kuuwa wanaume duniani,
ikiwa inasababisha vifo vya watu wapatao robo millioni kwa mwaka.
"wanaume wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya
kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60
ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa.
0 comments: