Mambo ya muhimu ya kutekeleza kisheria
kabla ya kuanzisha biashara ni:-
(a) Kuwa na ofisi
(b)
Kukata leseni
(c)
Kusajiliwa na TRA kama mlipokodi na kupewa namba ya mlipakodi
(d)
Kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya awali
(e)
Kutimiza masharti mengine ya keshiria kuwa mfano kama wewe unataka kufanya
biashara ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo lazima usajiliwe kwenye Bodi ya
Wakandarasi.
Kama
unafanya biashara ya kati au kubwa unapaswa kufuata sheria. Ni makosa kufanya
biashara bila kufuata sheria za nchi. Hata hivyo, kuna biashara zingine ndogo
ndogo sana kiasi kwamba uanzishaji wake si rahisi kufuata sheria hizo hapo juu,
Mfano
uuzaji wa maandazi, karanga na vitu vingine vidogovidogo. Hizi zinaitwa
biashara zisizo rasmi au biashara ndogondogo.
Ni vyema ukachunguza kama biashara unayoifanya
ni ndogo au kubwa ili ujue kama unapaswa kufuata taratibu za kisheria au la,
kwani kutokujua utaratibu na sheria siyo kinga ya kukufanya usishitakiwe.
0 comments: