Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto.
Katika
kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango
yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia
yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya
kisiasa, teknolojia, na uchumi.
Tengeneza
malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima
uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina
ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata.
0 comments: