Tengeneza orodha ya vitu
anavyotaka kufanya siku ya leo asubuhi ukiamka. Mara nyingi unapaswa kujua
mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni
usiwe na viporo.
Katika orodha yako tenganisha
orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata
usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako.
kujua kipi cha lazima ni moja ya
njia kubwa ya kupunguza gharama, kupoteza muda mwingi kwa vitu visivyo ya maana
na msongo wa mawazo.
Wanasema siku ya kesho inajengwa
leo usiku mipango yako yote na jinsi utakavyo panga na sio unaamka asubuhi ndio
unaanza kupanga ratiba yako au hujui kabisa siku hiyo utafanya nini..
0 comments: