Faida za mwanga wa jua ni nyingi:
1. Dakika kumi na tano hadi 30 za kupata mwanga wa jua kila siku katika ile sehemu ya mwanzo ya asubuhi au baadaye mchana alasiri husaidia mwili kukusanya pamoja au kutengeneza Vitamini D yake wenyewe, kirutubisho muhimu/homoni ndani ya ngozi.
Vitamini D huisaidia damu kutengeneza kalisi (calcium) na fosforasi, inayoijenga na kuitengeneza mifupa.
2. Mwanga wa jua unafanya kazi yake kama dawa ya kuvika viini vya maradhi na kuua vijimea vidogo sana (bacteria)
3. Jua linatoa nguvu ambayo kwa hiyo mimea inaweza kuigeuza kaboni dioksidi na maji kuwa kabohidreti [chakula cha wanga]… Bila ya njia hiyo wanyama na wanadamu wangekufa kwa njaa
4. Jua pia linamsaidia mwanadamu kujirekebisha na kukabiliana na kazi ya usiku na kupunguza unyong'onyevu (depression) unaotokana na siku za giza wakati majira ya baridi kali yanapotokea.
Neno la tahadhari: Mwanga wa jua unaweza pia kuleta madhara kukaa kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua kunaweza kuiunguza ngozi, kunaweza kuongeza hatari ya kupatwa na kansa ya ngozi kunaweza kuharakisha kuzeeka, kunaweza kuyaharibu macho.
0 comments: