Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Je..!!! Upo Tayari Kufunga Ndoa na Je wajua vigezo vya kuwa tayari kufunga ndoa...? Soma hapa..!!!!





Ili uweze kujibu swali hilo, unahitaji kujielewa vizuri. Kwa mfano, fikiria mambo yafuatayo:

Mahusiano. Wewe huwatendeaje wazazi wako na ndugu na dada zako? Je, mara nyingi wewe hushindwa kujizuia unapokuwa nao, labda hata kuzungumza kwa ukali au kwa kejeli?

 Wao wangejibuje ikiwa wangeulizwa swali hilo kukuhusu? Jinsi unavyoshughulika na watu wa familia yako huonyesha jinsi utakavyomtendea mwenzi wako.

Mtazamo. Je, wewe huwa na mtazamo mzuri au mbaya kuelekea mambo? Je, wewe hukubali maoni ya wengine, au nyakati zote wewe husisitiza mambo yafanywe kwa njia fulani—njia ile wewe unataka? Je, unaweza kuendelea kuwa mtulivu unapokabili hali ngumu? Je, wewe ni mwenye subira?

Gharama. Wewe hushughulikia pesa kwa njia gani? Je, mara nyingi wewe hujikuta ukiwa na madeni? Je, unaweza kudumisha kazi? Ikiwa huwezi, sababu ni nini? Je, tatizo ni kazi yenyewe?

Je, tatizo ni mwajiri? Au je, ni kwa sababu ya zoea au tabia fulani unayohitaji kufanyia kazi? Ikiwa ni vigumu kwako kushughulikia gharama zako mwenyewe, utashughulikiaje za familia yako?

Hali ya Kiroho. Una sifa gani za kiroho? Je, wewe husoma Neno la Mungu, kushiriki katika huduma, na kutoa maelezo katika mikutano ya Kiroho? Yule utakayefunga ndoa naye anastahili kuwa na mwenzi mwenye nguvu kiroho.

Kadiri unavyojielewa, ndivyo utakavyoweza kumpata mtu atakayekusaidia kukuza sifa zako nzuri badala ya udhaifu wako.


 

0 comments: