Kila wakati kumbuka kuwa “Hata wao
walianza kama sisi” nasi ipo siku tutakua kama wao na zaidi ya wao, kielimu,
kimaisha, kiuchumi, kiutamaduni, kimichezo, kibiashara n.k kwani wao nao ni
binadamu kama sisi; asiwepo mtu wa kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa na mtu
awaye yote,
Kaa kwenye eneo lako na boresha
karama (kipawa) ulichonacho; kwani kila mtu ana maisha yake na hata sasa ukweli
wa kauli hii “kila mbuzi atakula kutokana na urefu wa kamba yake” haujabadilika
na unatenda kazi ipasavyo ukiwa na maana ya kila mtu atafanikiwa kulingana na
juhudi zake katika kazi. jijukumishe ndugu yangu.
Maeneo yafuatayo uonyesha jinsi watu
mbalimbali (wao) walivyofanikiwa na namna unavyoweza kufanikiwa zaidi yao; soma
kwa makini na fuatilia jambo linalokuhusu ili ufanikishe ndoto zako kwa muda na
wakati sahihi:-
Elimu
Biashara
Ndoa
Uongozi
Utumishi-Huduma
Utajiri/Mali
Kazini/Vyeo
Afya
Michezo/ Sanaa
Kijamii
Maisha baada ya shule
Urembo/ utanashati
Ujasiriamali
Kilimo na mifugo
Ishi maisha yako ya asili kama
ulivyo-umbwa, acha kuishi maisha ya watu wengine na ongeza uwezo wako wa
kujiamini kwa kuwa na maarifa ya kutosha na taarifa sahihi katika kila jambo
ufanyalo chini ya jua, lakini tambua ya kuwa “ujana ni ubatili na utu uzima
pia” hivyo katika kila unalolifanya mtangulize Mungu kwanza.
asante sana kwa hayo
ReplyDeleteMaranyingi walio fanikiwa huwa hawasemi mbinu sahihi yaliyopitia kufkia mafanikio yao; naww broo jitahind kufafanua vizur mada zako zieleweke vzur lazima uweke mifano ya watu waliofanikiwa na utaje wametokea familia yenye uwezo gn wa kifedha ili tukuelewe
ReplyDelete