Migogoro
ya kifamilia ni changamoto kubwa na hutokea pale mwanafamilia anapokuwa na
mtazamo tofauti wa mawazo na mwanafamilia mwingine. Mara nyingi migogoro ya
familia hutokea kwa misuguano midogo na kukimbilia katika uamuzi usiofaa.
Kukwaruzana
kusiposhughulikiwa kwa muda muafaka husababisha migogoro na mifarakano
mbalimbali ndani ya familia. Kuna njia mbalimbali za mawasiliano zinazolenga
kurejesha amani na upendo ndani ya familia. Njia hizo ni makubaliano ya pamoja
au kukubali kwa kutokukubaliana.
Kwa
nini migogoro ya kifamilia inazidi badala ya kupungua?Zipo sababu nyingi
zinazochangia kuongezeka kwa migogoro ya familia. Baadhi ya sababu hizo ni:
Kuishi katika nchi maskini. Umasikini wa nchi hasa wa kipato ukitafsiriwa katika ngazi
ya familia uonekane mkubwa kwani mahitaji muhimu (chakula, mavazi, hifadhi)
huongezeka na kipato ndani ya familia hupungua.
Hali
hii huchangia kwa wanafamilia kutokuelewana kwa sababu ya maisha magumu kila
siku na wakati huo huo pengo la familia za walionacho na wasionacho likizidi
kuongezeka.
Ongezeko la familia. Hali ya kujifunza kuishi kifamilia, kuzaliwa kwa
watoto, kuongezeka kwa mahitaji na matumizi muhimu ya kifamilia ni sababu
nyingine inayochangia kuongezeka kwa migogoro ya familia.
Ukosefu wa uaminifu. Kukosekana kwa uaminifu mara nyingi huwa ni chanzo
cha mifarakano ya kifamilia katika jamii. Matumizi ya maneno yanayojenga
uhusiano mwema ndani ya familia kama vile; ‘niamini’, ‘nakupenda’, nisamehe,
nivumilie na mengine mengi kama hayo.
Maneno
hayo husaidia kudumisha amani na upendo katika familia. Ukosefu wa uaminifu
huharibu uhusiano, uwajibikaji na mbaya zaidi husababisha kutoaminiana miongoni
mwa wanafamilia.
Ufahamu mdogo wa maisha ya familia. Uhusiano wa kifamilia ni changamoto kwa kila mtu bila
kujali jinsia, kipato, au kiwango cha elimu. Hivyo inatakiwa kusoma vitini vya
uhusiano na kuomba ushauri kwa wenzetu wenye uzoefu zaidi katika masuala ya
kifamilia. Kwa mfano, wanafamilia wachanga wanashauriwa kutumia wazee katika
masuala ya ndoa na malezi ya familia.
Uelewa
mdogo, kukaa sehemu moja, hasira, jazba, matumizi ya nguvu, ulevi kupindukia,
talaka, ulafi, vipigo, kutelekeza familia, kutumia muda mwingi kazini, na
mengine mengi ambayo hatutakiwi kudharau ili kujenga familia imara na zenye
mahusiano mema.
mafundisho ni mazuri mno na kuna sababu nyingine kama vile kunyimana tendo la ndoa na umasikini uchangia kwa kiasi kikubwa lakini pia kuingia katika maswala ya familia kwa maana ya kuoa na kuolewa bila elimu ya maswala hayo AKSANTE KWA MADA NZURI!
ReplyDelete