Ni
vizuri kujizoesha kutafakari kuhusu wewe ni nani, mapungufu yako, mambo gani
makubwa na mazuri uliyokwisha wahi kufanya, na vitu gani hasa unavipenda na
usivyovipenda.
Tafakari
hii itakupa picha ya aina gani ya mtu wewe ulivyo, na kukusaidia kujipanga
kuziba yale mapungufu, na wakati huo huo, utaweza kuangaza fursa zilizopo na
unazoweza kuzitumia kutokana na 'ubora' ulionao.
Tafakari
hii itakuwezesha pia kutambua kitu kiitwacho kwa kiingereza 'passion', yani
mambo unayoyapendelea sana kufanya au kuwa hapo baadae. Umuhimu wa kutambua
passion ni kwamba ukiweza kuwekeza muda katika passion yako inaweza kuwa sehemu
nzuri ya kujijengea maisha yenye furaha.
Kwani passion itakufanya ufanye jambo
utalotaka kulifanya kwa ufanisi na pia hata ukikumbana na changamoto, hautokata
tamaa kirahisi rahisi.
0 comments: