Miongoni
mwa sababu kubwa zinazosababisha wengi kutotimiza malengo waliyojipangia kwa
muda stahiki ni pamoja na kushindwa kusimamia anachokitaka.
Unakuta mtu mmoja ana mipango lukuki
kichwani kwa wakati mmoja. Mathalani unakuta mtu anawaza kuanzisha mradi wa
kufuga kuku, lakini wakati huohuo anawaza jinsi ya kuanzisha duka kubwa au
kufungua shule ya awali.
Yote hayo anawaza kuyatimiza kwa
wakati mmoja. Si jambo sahihi na maisha hayawezi kuendeshwa na kutimizwa kwa
mtindo ama mlengo huo.
Tambua unachokihitaji, pigania kukipata na uwe na msimamo wa kifikra juu ya jambo hilo.
Tambua unachokihitaji, pigania kukipata na uwe na msimamo wa kifikra juu ya jambo hilo.
Asante sana kwa elimu nzuri
ReplyDeleteVizuri sana kwa kuelimisha jamii
ReplyDelete