Jambo linalosababisha biashara zisiendelee ni pale mhusika anaposhindwa kupata soko la uhakika. Unaweza kuzalisha bidhaa za viwango vya juu pamoja na kutafuta masoko kwa wingi, lakini ukawa hauna soko la uhakika.
Utafiti
unaonesha kuwa, wafanyabiashara wengi wanaanza biashara kwa kufanya utafiti wa
juu juu bila kujiridhisha uhitaji wa biashara anayotaka kuianzisha kama atapata
wateja au la. Matokeo yake anatumia mtaji mkubwa, muda na nguvu wakati huo
biashara hiyo inakuwa na faida ndogo.
Nini kifanyike? Kabla ya kuanza biashara inatakiwa ufanyike utafiti wa kutosha wa kujua kama soko litakuwapo, ukubwa wa soko hilo na uimara wake. Huhitaji kufanya utafiti wenye gharama kubwa. Unatakiwa kuzungumza na wateja wako kwa kuwauliza ni kwa kiasi gani wananunua bidhaa hizo na mara ngapi.
Zungumza na wasambazaji na washindani wako. Jua biashara nyingine zinakwenda vipi na jinsi gani wanaboresha masoko yao. Kushindwa kwa bidhaa inawezekana inatokana na kushindwa kwa biashara. Sababu ya kushindwa kwa bidhaa inawezekana ni kutokana na maelezo ya mfanyabiashara husika, bidhaa yenyewe au soko.

0 comments: