Kila kitu huanza na kitu Fulani hata kama ni kidogo sana,
kuwa na duka kubwa la bidhaa huanza na mtaji mdogo sana ambao maamuzi yake
hutegemea na malengo na vipaumbele vya mfanya biashara, mwenye duka angeweza
kuutumia huo mtaji kataka matumizi ya nyumbani au kuchangia harusi ya rafiki
yake na asiwekeze katika duka.
Kitu alichokuwa nacho ni wazo la kufanya biashara na hilo
ndilo lililo mpelekea kupata mtaji ambao umemfanya awe na duka la bidhaa wakati
huu
Kuna nguvu isiyo-onekana iliyo mfanya awe na kitu tunacho
kiona kwa macho ya nje na hiyo nguvu isiyo-onekana kila mtu anayo, kwani huwezi
kuishi bila kuwa nayo na Mungu ameiweka ndani yetu.
Nguvu
isiyo-onekana. Hii ni nguvu ambayo mwanadamu
ameumbiwa nayo ili kumwezesha afanye kazi na kuishi kwa kujitegemea mwenyewe.
kila mtu anayo hata awe mtoto wa mwezi mmoja, kwa mfano:- nguvu ya kuona imo
kwenye macho ya mwanadamu na mnyama, nguvu ya kutawala na kusimamia mambo
mbalimbali imo ndani yetu lakini hatuioni kwa macho ya nyama ila tunayo.
Hivi umewahi jiuliza kwa nini baada ya kula chakula huwa
unaenda kujisaidia haja kubwa au ndogo? Au kwa nini njaa ikikuuma huwezi
kuendelea na shughuli zingine mpaka umepata chakula? Hebu sema niliishiwa nguvu
mwilini lakini baada ya kula nikapata nguvu na kuendelea kufanya kazi!
Tuiangalie hiyo nguvu isiyo-onekana kwa kina ili tuweze
kutumia kile tulicho-nacho kupata kile tunacho kihitaji.
0 comments: