Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Je..!!!! WAJUA UKIWABAINI ADUI ZAKO UFANYE NINI … SOMA HAPA



Jambo La Msingi La Kufanya Pale Tunapobaini Kuwa Kuna Watu Wanaotuchukia Mahali Popote Pale, Ni Kutumia Njia Zifuatazo;

KWANZA: Ni Kufunua Ukweli Kuhusu Kuchukiwa, Yaani Tuwaambie Wanaotuchukia Kuwa Hatufurahishwi Na Chuki, Tuwaombe Msamaha Ikibidi.

PILI: Tujilinde Wenyewe Kwa Kupunguza Uhusiano Na Mwingiliano Wa Kimatendo Na Kauli Hasa Zenye Kupingana.

 TATU: Tutumie Muda Mwingi Sana Kuambatana Na Wanaotupenda Na Kupata Faraja Kwao, Lengo Ni Kuharibu Hisia Mbaya Zitakazokuwepo Kwenye Akili Zetu Juu Ya Wanaotuchukia.

NNE: Tusiachie Nafasi Za Kimaisha Wazitawale Adui Zetu; “Mimi Sitafanya Kazi Na Fulani Acha Afanye Yeye Aone Raha.

“Nitaacha Kazi Ili Tusigombane Naye Zaidi.” Kamwe Tusitoe Nafasi Za Utawala Badala Yake Tuonyeshe Wengine Kwamba Tunatekeleza Majukumu Yetu Ya Kimaisha Vizuri Ingawa Tunachukiwa Kwenye Familia Au Kazini.

TANO: Tuwashirikishe Ndugu/Rafiki Wenye Busara Katika Kila Kwazo Ili Wasaidie Namna Ya Kufanya. Tusichukue Uamuzi Wenyewe Bila Ushauri Hasa Tunapokuwa Na Hasira. Tujipe Muda Wa Kutafakari Zaidi Kila Jambo La Chuki Tunalofanyiwa Kabla Ya Kuamua Kufanya Chochote.

MUHIMU: Tuepuke Kukuza Mgogoro Kwa Kuwajumuisha Wengine Kwenye Ugomvi. Tusikumbatie Tatizo Na Kulikuza Kwenye Mawazo Yetu. Tuwe Watu Wa Kupuuza Na Kupunguza Msongo Wa Mawazo.


0 comments: