Hapa ndipo watu wanapotakiwa kutumia akili zao mpaka zile za akiba, ukikosea hapa ni rahisi sana kuvurunda hapo baadaye. Uhusiano wenye nguvu, hujengwa na penzi la kweli. Acha kukurupuka, lazima ujihakikishie kwamba uliyenaye ni chaguo kutoka ndani ya moyo wako.
Mwenzi ambaye unatarajia kuwa naye
katika maisha ya ndoa hapo baadaye, lazima msingi uwe ni uchaguzi sahihi. Sikia,
watu wengi waliokuwa na fedha, wamefilisika baada ya kuoa/kuoleawa na wenzi
ambao si sahihi.
Aidha, wapo wenye mafanikio makubwa sana,
ambayo wameyapata baada ya kuoa/kuolewa na wenzi sahihi. Rafiki zangu, si jambo
rahisi kumpata yule aliye sahihi. Inahitaji utulivu.
Yapo mengi sana ambayo unapaswa kuyaangalia, ambayo nimekwishaeleza sana katika makala zangu zilizopita. Wakati nahitimisha kipengele hiki, shika neno moja tu; unapomchagua mwenzi wa maisha yako, hakikisha ni yule aliye sahihi!
0 comments: