Baada
ya kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya
biashara ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako
upoje, na wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika.
Biashara
inahusu kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa
kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze
kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa
endelevu.
Kinyume
cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia kwa
wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata wateja
na kuendelea kupanua biashara.
Inabidi
uipende shughuli husika unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja
kupitia biashara husika.
Muda
wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama
ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi
‘haikuboi’.
0 comments: